19 Machi 2011 - 20:30

Tukio la mwanamke mmoja wa Ufaransa kujifungua mtaani mjini Parislimezusha hasira na malalamiko makubwa ya wananchi na jumuiya za kupambana na umaskini nchini humo

Ripoti ya Shrika la Habari la AhlaulBayt(a.s)ABNA:Habari zinasema kuwa mwanamke huyo anayelala kwenye maboxi alijifungua jana katika mtaa mmoja wa Paris bila ya msaada wa aina yoyote na kwamba wahudumu walipofika hapo mtaani walikuta mtoto wa kike wa mama huyo amefariki dunia na kufanikiwa kuokoa maisha ya mama huyo maskini pekee aliyekuwa pamoja na mumewe.Jumuiya ya Kupambana na Vifo Mitaani nchini Ufaransa imesema matukio kama hayo ya kufariki dunia mama wajawazito wanaojifungua mitaani ni matokeo ya siasa mbaya za serikali ya Paris za kupuuza watu maskini wasiokuwa na makazi. Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mpaka pia imeripoti kuwa siasa mbaya za serikali ya Ufaransa zinawazuia watu maskini kupata huduma za afya.Ripoti ya Jumuiya ya Kupambana na Vifo Mitaani ya Ufaransa inasema kuwa tokea manzoni mwa mwaka huu wa 2011 watu 280 wamefariki dunia mitaani kutokana na umaskini nchini Ufaransa