19 Machi 2011 - 20:30

Kijana mwingine anayejulikana kwa jina la Ali al Filfil ameuawa kwa kupigwa risasi na maafisa usalama wa Saudi Arabia katika mji wa al Qatif wa mashariki mwa nchi hiyo.

Ripoti ya ABNA: Ukurasa wa Intaneti wa televisheni ya al Alam umeripoti kuwa, kijana huyo ameuawa baada ya maafisa usalama wa utawala wa ukoo wa Aal Saud kuwafyatulia risasi na mabomu ya kutoa machozi waandamanaji waliokuwa wanataka wakabidhiwe mwili wa kijana mwingine aliyeuliwa na maafisa hao hivi karibuni.Kijana huyo aliuliwa "kwa damu baridi" mjini Qatif baada ya kupigwa risasi na askari wa Saudia wakati alipokuwa njiani kurejea nyumbani kwao.