ABNA inatuarifu kuwa:Maazimio hayo yaliyopasishwa kwa wingi wa kura dhidi ya Israel, yamelaani hatua za utawala wa Kizayuni za kukiuka kwa kiasi kikubwa haki za binadamu za wananchi wa Palestina na hasa katika Ukanda wa Gaza. Moja ya maazimio hayo limepinga ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina na kueleza kuwa, ujenzi wa vitogoji hivyo katika eneo la Baitul Muqadas Mashariki na pia ukuta wa kibaguzi ni mifano ya wazi ya ukikaji haki za binadamu kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa. Maazimio hayo yalipigiwa kura za hapana za Marekani, Canada na baadhi yake Australia. Hayo yamejiri ikiwa wiki 3 zimebakia kabla ya kufanyika mkutano wa kamati ya 4 ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wa kulaani hatua za Israel za kukiuka haki za binadamu za wananchi wa Palestina.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 283162
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepasisha kwa pamoja maazimio 9 yanayopinga jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu.