Rais Abdul Aziz Boutefliqa wa Algeria ametuma pongezi zake kwa Munsif al Marzouq kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Tunisia tangu wananchi wa nchi hiyo walipompindua dikteta Zainul Abidin Ben Ali.Rais Boutefliqa pia amesema katika katika ujumbe wake wa pongezi kwamba ana matumaini Rais mpya wa Tunisia ataweza kutekeleza vizuri matakwa ya wananchi wa nchi hiyo.Munsif al Marzouq ambaye alikuwa mpinzani mkubwa wa dikteta Zaynul Abidin Ben Ali, alipendekezwa na chama cha Kiislamu cha an Nahdha kugombea nafasi hiyo ambapo jana Jumatatu, wajumbe wa Baraza la Waasisi wa Tunisia walimteua kuwa Rais mpya wa nchi hiyo.Baraza la Waasisi wa Tunisia lina wajumbe 202, ambapo Munsif al Marzouq amechaguliwa kwa kura 153 za wajumbe wa baraza hilo.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 283865
Rais Abdul Aziz Boutefliqa wa Algeria ametuma pongezi zake kwa Munsif al Marzouq kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Tunisia tangu wananchi wa nchi hiyo walipompindua dikteta Zainul Abidin Ben Ali.