19 Machi 2011 - 20:30

Matokeo ya awali ya zoezi la kuhesabu kura nchini Misri yanaonyesha kuwa vyama vya Kiislamu vinaongoza katika awamu hii ya pili ya uchaguzi wa bunge.

Matokeo ya awali ya zoezi la kuhesabu kura nchini Misri yanaonyesha kuwa vyama vya Kiislamu vinaongoza katika awamu hii ya pili ya uchaguzi wa bunge.Matokeo yaliyotangazwa Ijumaa yanaonyesha kuwa Chama cha Uhuru na Uadilifu cha Harakati ya Ikwanul Muslimin kinaongoza.Nao mrengo wa kiliberali wa Misri unashika nafasi ya tatu baada ya chama cha Kisalafi cha An-Nur. Awamu ya pili ya uchaguzi wa bunge Misiri ulifanyika Jumatano na Alhamisi katika mikoa 10. Awamu ya tatu ya uchaguzi wa bunge utafanyika mapema Januari ambapo vyama vya Kiislamu vinatazamiwa kupata ushindi zaidi. Awamu ya kwanza ya uchaguzi wa bunge ilifanyika Novemba 28 ambapo vyama vya Kiislamu pia vilipata ushindi mkubwa.