Watu 19 wameripotiwa kuuawa katika mapigano kusini mwa Somalia, kati ya wanamgambo wa al Shabaab na askari wa serikali ya mpito ya nchi hiyo. Kundi la al Shabaab limedai kuwa liliua askari 11 wa serikali ya Mogadishu na kujeruhi makumi ya wengine jana Ijumaa katika eneo la Gedo, kusini magharibi mwa nchi hiyo. Naye Kamanda wa jeshi la Somalia katika eneo la Gedo, Muhammad Abdi Kalil amesema askari wa serikali ya mpito ya Somalia wameua wanamgambo 8 wa al Shabaab kwa kuwamiminia risasi.Eneo la Gedo ambalo liko katika mipaka ya nchi hiyo na Ethiopia na Kenya, limekuwa chini ya udhibiti wa al Shabaab tokea mwaka 2009.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 284635
Watu 19 wameripotiwa kuuawa katika mapigano kusini mwa Somalia, kati ya wanamgambo wa al Shabaab na askari wa serikali ya mpito ya nchi hiyo.