19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 285773
ABNA inatuarifu kuwa:Wakazi jijini Dar es Salaam, Tanzania wameendelea kukadiria hasara iliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha hapo jana.
Mamia ya wanabiashara wamesema wamepoteza mali mzomzo kufuatia mvua
hiyo. Baadhi ya wakaazi wa mji huo wameiambia idhaa hii kwamba mvua
hiyo ilikuwa kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu Tanzania ijipatie
uhuru wake. Habari zaidi zinasema kwa uchache watu 13 wamekufa maji
kutokana na mvua hiyo. Miongoni mwa waliofariki dunia ni mtoto mdogo
mwenye umri wa miaka 6. Madaraja yanayounganisha jiji la Dar es Salaam
na maeneo mengine yamesombwa na maji huku nyumba kadhaa zikiporomoka
kufuatia mvua hiyo.