Akizugumza na waandishi wa habari kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe; Wizara yake imepata taarifa hizo ambazo zimezagaa jijini Dar es Salaam, zinazoeleza kuwa kundi moja linalotarajiwa kushiriki katika mpango huo ni la wazee kutoka Kisiwa cha Pemba, wanaotaka kisiwa hicho kijitenge. Membe alieleza kuwa, taarifa zinaonyesha kuwa wazee hao wamepanga kuwa na mabango ya kumkashifu Muheshimiwa huyo kwa madai kuwa ni mnyanyasaji wa haki za binadamu kutokana na ombi lao kukataliwa na shirika lililo chini ya uongozi wake. Wazee hao wamepanga kulala barabarani katika maeneo ya Buguruni, njia ambayo anatarajiwa kupita Ki-Moon na endapo watafanikiwa kuusimamisha msafara wa kiongozi huyo, watamsomea risala yao juu ya azima yao ya kutaka Kisiwa cha Pemba kijitenge. Membe alisema serikali haijazipuuzia tetesi hizo na imejipanga vilivyo kuhakikisha wale wote waliopanga kuihujumu ziara ya katibu mkuu huyo hawafanikiwi. “Tunawaomba Watanzania waonyeshe ukarimu, matatizo yao wayamalize wenyewe na wasiitumie ziara hii kwa mambo yasiyofaa.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 289513
Kufika kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-Moon nchini Tanzani juma tatu, kwa ziara ya siku tatu, serikali imefichua mpango wa baadhi ya Watanzania kuvuruga ziara yake hiyo.