Shutuma hizo ambazo hapo awali zilidai ya kuwa watu saba walio kuwa karibu ya rais Paul Kagame ndiyo waliohusika katika kuangusha ndege hiyo na kupelekea kufunguliwa kwa kesi hiyo kwani katika ajali hiyo walikuwepo raia wa Kifaransa. Wachunguzi watoa repoti kwa kusema " uangushwaji wa ndege iliyokuwa imebeba rais Juvenal Habyarimana iliangushwa na wanajeshi wa waliokuwa ndani ya serikali." Waziri wa mambo nchi za nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo alisema " ukweli uliopatikana umethibitisha ya kuwa watu walioshutumiwa hawakuhusika katika kufanya kitendo hicho na serikali ya Rwanda ilisha kanusha madai hayo ya kuhusika katika kuangusha ndege hiyo." Hapo awali mwaka 2006 serikali ya Ufaransa ilitoa kibali cha kukamatwa watu hao saba wakiingia Ufaransa, jambo ambalo lilipelekea uhusiano kati ya Rwanda na Ufaransa kuzorota hadi mwaka 2009 ulipo anza kuimarika.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 290046
ABNA inatuarifu kuwa:Wachunguzi walio kuwa wanachunguza uangukaji wa ndege iliyo muua rais wa Rwanda 1994 Juvenal Habyarimana, wamethibitisha ya kuwa serikali ya sasa ya Rwanda haikuhusika katika hujuma ya ndege hiyo.