4 Machi 2012 - 20:30

Jaafar Sayyid Salman Jumaa Alawiy mkazi wa Mkoa wa Ash sharukhah Bahrain kwa athari ya kipigo kikali na Polisi wa Bahrain, aliaga Dunia kwa athari ya majeraha ya kichwani mwake.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Jaafar Sayyid Salman Jumaa Alawiy mkazi wa Mkoa wa Ash sharukhah Bahrain leo asubuhi alikabidhi roho kwa athari ya kipigo kikali na Polisi wa Bahrain.

Shahidi huyu mwenye Umri wa miaka 75 baada ya kupigwa vikali kichwani mwake na athari ya pigo hilo Fuvu lake lilivunjika na ikawa sababu ya kuiaga Dunia kwa kipigo hicho.

Vijana wa mapinduzi ya 14 February walisema: pamoja na uzee wa shadihi huyu alikuwa sambamba nasi katika maandamano yetu na kushiriki katika kila maandamano yote.

Shahada ya mkazi huyu wa Mkoa wa Ash sharukhah Bahrain iliongeza idadi ya Mashahidi kufikia 73.

Kutona na shahada hii Maulamaa akiwemo Ayatullah Shaekh Issa Qasim na Sheikh Al gharifiy katika hotuba zao leo walilaani mauaji hayo na kuomba Wananchi kuandama Ijumaa ijayo kwa wingi kupinga mauaji yanayoendelea Bahrain.