13 Machi 2012 - 20:30

ABNA inatuarifu kuwa: Shirika moja la uchunguzi wa maswala ya siasa limetoa habari kuwa aliyekuwa rais wa Libya Muaamar Gaddafi alichangia pesa kusaidia kampeni za uchaguzi wa Sarkoozy rais wa Ufaransa.

habari za shirika hilo zinasema "kiasi cha Euro 50 million zilitolewa kwa rais wa sasa wa Ufaransa Nicolas Sarkozy  na rais wa Libya Muammar Gaddafi kabla ya kuangushwa kutoka madarakani."Hata hivyo rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy alikanusha madai hayo kwa kusema " nafikri mnajua kuwa Gaddafi alikuwa akiongea atakalo na habari hizi hazina ukweli wowote."Uhusiano wa rais Sarkozy wa Ufaransa na rais Gaddafi wa Libya ulikuwa wa karibu sana lakini hatimaye urafiki uligeuka uhasimu.