Ripoti za kuaminika zinaashiria hali mbaya ya Husni Mubaraka, kutokana na hali mbaya alokuwanayo Madaktari wa Mubaraka nao wameelezea kusubiri kwao Qudra ya Mungu. Madaktari hao wameeleza kuwa Mubaraka ameomba kukutana na watoto wake wakiume( Jamali na Alaau) ambao wapo katika jela ya Tareh, na mkewake pia wajukuu zake, imelezwa kuwa Alaau na Jamali walikwenda kuonana na baba yao baada ya kuruhusiwa na jela hiyo kwa muda wa masaa mawili. Kutokana na mazingira haya yawezekana kuwa Mubaraka yuko katika hali ya maututi.Raisi wa zamani wa Misri anasumbuliwa na maradhi mbali mbali ikiwemo maradhi ya Kansa ambayo imepelekea kuuathirika vibaya mwili wake, lakini yapaswa kufahamika kuwa simara ya kwanza kwa Mubaraka kufikia hali hii.
31 Machi 2012 - 19:30
Msimbo wa Habari: 305765
Vyombo vya habari vya Misri vimetangaza hali mabaya ya Raisi wa zamani wa nchi hiyo (Husni Mubaraka) na kuwa yuko katika hali ya umaututi.