Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA-Mwanazuoni maarufu wa Nchi ya Bahrain Ayatullah Sheikh Issa Qasim alisema: Katika Nchi ya Bahrain hakuna uhuru kwani kauli ya kwanza ni utawala na Wananchi hawana haki ya kuongea dhidi ya utawala.
Akiendelea kusema: Utawala wa Alikhalifa Bahrain wafasiri Dini kwa matakwa yake, na kuipa Dini kila maana watakayo na kuona nadharia zao kuwa bora kuliko za wengine na Misikiti iliosimama dhidi ya utawala huo huvunjwa na kila wito wa kudai uhuru hatimae ni kuhukumiwa vikali.
Ayatullah Sheikh Issa Qasim aliendelea kusema: Misikiti ilokuwa mingi ya Bahraini imekwisha kuvunjwa na Misikiti ilobaki pia hatima yake itakuwa ni hiyo hiyo, na mahudhurio ya Swala katika Misikiti hiyo imekuwa ya kuzorota kwani Waumini wanaoswali katika Misikiti hutuhumiwa kwa makosa ya kuwa dhidi ya utawala wa Bahrain.
Chama cha Wananchi cha Al-Wafaq kilitoa ujumbe wake kwa kutiwa mbaroni Muhammad Nabiil Rajab mwanadiplomasia wa Nchi hio.
Katika ujumbe huo kumeelezwa kuwa; Kushikwa Muhammad Nabiil Rajab ni ishara ya kuonyesha kuwa utawala wa Bahrain hauwapi Wananchi uhuru, na kuwa kinyume na matakwa ya Jumuiya ya Kimataifa kwa kuachiwa huru wafungwa wa Kisiasa Nchini humo.
Al-Wafaq: Kuendelea kushikwa Wananchi wasokuwa na hatia na kutiwa mbaroni wanasiasa ni kusababisha machafuko Nchini, na bila kufikiria hatima ya mambo machafu wanayo wafanyia Wananchi itakuwa nini.
Al-Wafaq: Kushikwa Muhammad Nabiil Rajab na wafungwa wengine ni kuonyesha kuwa utawala wa Bahrain imeenda kunyume na matakwa ya Nchi 45 zilizokubaliana na utawala wa Bahrain kutoshika Wanasiasa na Wananchi wasokuwa na hatia.