Takwimu hizi zimetolewa na shirika la kiuchumi la Eurostat ambalo limesema uchumi katika mataifa 17 yanayotumia sarafu ya Euro umeshuka.
Hata hivyo, uchumi wa Ujerumani umekua kwa aslimia 0 nukta 3 kwa kipindi cha robo wa mwaka wa pili mwaka huu.
Wataalam wa uchumi nchini humo wanasema uchumi huo umeimarika kutokana na bidhaa na mazao yanazosafirishwa nje ya taifa hilo na pamoja na kutumia bidhaa za nyumbani.
Wakati Ujerumani ikitangaza ongezeko hilo, Ufaransa nayo imetangaza kuwa uchumi wake haujakua kwa kipindi hicho kinyume na ilivyotarajiwa kutokana na uongozi mpya kuingia madarakani.
Aidha, uchumi wa Ufaransa haijaonesha kukua kwa kiwango chochote kuanzia mwanzo wa maka huu.
Hata hivyo, uchumi wa Ujerumani umekua kwa kiasi cha chini kinyume na asilimia 0 nukta 5 iliyoshuhudiwa mapema mwaka huu.
Licha ya uchumi huo kuimarika, watalaam hao wa uchumi wanasema pia huenda uchumi wa Ujerumani ukashuka zaidi kutokana na hali ngumu ya kiuchumi katika mataifa ya bara Ulaya.