17 Novemba 2012 - 14:12

Mapambano kati ya Palestina na Israel leo tarehe 17 yameingia katika siku ya nne, ambapo ndege za kijeshi za Israel zinaendelea kupiga mabomu dhidi ya maeneo kadhaa yaliyolengwa katika sehemu ya Gaza, na kusababisha vifo vya wapalestina wanne, na wengine 30 kujeruhiwa.

Hadi sasa mapambano hayo yamesababisha vifo vya wapalestina 35, wakiwemo raia 10, na wengine wasiopungua 300 kujeruhiwa.

Ikulu ya Marekani tarehe 16 ilisema rais Barack Obama wa nchi hiyo amefanya mazungumzo kwa simu na viongozi wa Israel na Misri kuhusu hali ya wasiwasi ya Gaza, na kuzitaka pande zinazohusika zirejeshe utulivu haraka, ili kuepusha vifo na majeruhi ya watu wengi zaidi.

Rais Mohammed Morsy wa Misri tarehe 16 ametoa taarifa akisema Misri haitakaa kimya kuhusu hali ya Gaza, na operesheni ya kijeshi ya Israel katika sehemu hiyo ni uvamizi dhidi ya haki za binadamu.