kamanda wa jeshi la maji la Jamhuri ya kiislamu ya Iran Jeneral Amir Daryadar: ameelezea akisema: makombora haya; kombora la masafa marefu liitwalo "Qadir" na masafa ya kati liitwalo "Nur" ni makombora yenye uweza wa hali ya juu wa kuangamiza na uwezo wa hali ya juu wa kulenga shabaha bila kukosea, makombora haya yametengenezwa kukabiliana na nyambizi na manoari za aina zote. aliongeza kwa kusema: makombora haya yametengenezwa Iran chini ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislam ya Iran na teknorojia iliyotumika kutengeneza makombora hayo ni ya pekee kabisa.Kamanda huyo aliendelea kusema: makombora haya yamelizidishia jeshi la Iran uwezo maradufu, kwani makombora haya yanaweza kumuangamiza adui akiwa mbali kabla hata yakuikaribia Iran.
1 Januari 2013 - 20:30
Msimbo wa Habari: 377709
katika mazoezi ya kuonyeshwa uwezo wake wa kujihami na kulinda amani ya mashariki yakati, jeshi la Jamhuri ya kiislamu ya Iran limetumia makombora mapya mawili yenye uwezo wa hali ya juu.