Akizungumza mjini Manama, waziri wa usalama wa nchi Sheikh Rashid bin Abdullah Al Khalifa amesema watu wengine wanane pia walikamatwa kwa tuhuma za kuhusika na shughuli za maandamano. Utawala wan chi hiyo Al Khalifa umedai kua watu wanaoandamana nchini humo wanauhusiano na nchi za Iran, Iraq na Lebanon. Na kudai kua miongoni mwao walipokea mafunzo ya silaha na mabomu na kupata ufadhili kutoka nje ya Bahrain. Waziri huyo ameongeza kuwa hivi sasa mazungumzo ya kitaifa yanaendelea ambayo yanahusisha pande mbali mbali za kisiasa ikiwemo upinzani. Jana jioni vurugu zilishuhudiwa katika mji wa Budaiya ulio pwani kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, ambapo waandamanji walifunga barabara na kufanya uharibifu.
16 Februari 2013 - 20:30
Msimbo wa Habari: 391852
Watu wawili wameuawa na polisi 75 kujeruhiwa nchini Bahrain tangu vurugu zianze usiku wa mkesha wa maadhimisho ya pili ya maandamano ya kupinga serikali ya mwaka 2011 nchini humo.