Shirika la habari la AhlulBayt(a.s) –ABNA; Sheikh Mazhar Shahin Imamu wa msikiti wa Amru Mukaram amesifu juhudi za Sheikh wa Azhar katika kuwaacha huru wafungwa 150 wa kimisri waliokuwa wamefungwa katika jela za Emarati nakusema yeye amefanya kazi ambayo wengine wamishindwa kuifanya.
Pia alisema katika hutuba ya sala ya ijumaa; Sheikh amefanikiwa katika suala ambalo wengine hawakuweza kulifanikisha katika suala hilo, hivo Azhar inapaswa kuwa huru na kutofungamana na kikundi chochote cha kisiasa.
Shahin amelitaka jeshi la nchi hiyo kuwa wasimazi wa chakula cha wanachuo cha Azhar kwaaminajili ya kusimamia suala la chakula na kuto tokea suala la sumu kuwekwa katika chakula hicho hatimae kupunguza na kuishusha Shahsia ya Sheikh wa Azhar.
Vilevile amewataka viongozi wa kisiasa kuwa; vyombo vya kisheria kutokuwa mbali na harakati za kisiasa kwalengo la wananchi kutopoteza imani ya chombo hicho muhimu, kwani kama Azhar na vyombo vya kisheria vitaangunka Serikai nayo pia itaanguka.
Mafunbo haya yameelekezwa kwa Muhammad Mursiy Rais wa jamhuri ya Misri na kikundi cha Ikhwanul Muslimina pia maelezo hayo yaliungwa mkono na waumini waliohudhuria katika ibada ya sala msikiti humo.
Naye aliendelea kusema kuwa; kuna badhi ya watu wafikapo madarakani mamilioni ya watu kukosa kazi watu ambao waliziweka roho hatarini kwaajili ya kufika kwao madarakani, hata baadhi yao walipoteza maisha katika viwanja vya Tahriri pia na wengine kujeruhiwa, hata baadhi ya majeruhi hao bado wapo Hospitali mpaka sasa, lakini waliowatetea kupata uongozi hivi sasa wamesha wasahau.
Pia katika kumkosoa Muhammad Mursiy Rais wa jamhuri ya Misri kwasababu ya Lugha mbovu na watu wanaosema kweli alisema siasa ya kuwaweka watu na njaa ikiwa ni dhidi ya wanaompinga nikitu kisicho kubalika.
Mwisho alisistiza umoja baina ya wananchi wa nchi hiyo na vikundi vyote vya kisiasa vya nchi hiyo mfano wa Masalafia na Ikhwanul Muslimina na aliwataka kuwataja waliofanya mauaji ya wanajeshi wa kimisri katika mipaka ya Rafah