Bw. Ryabkov amesema, hivi sasa maoni tofauti ya nchi hizo mbili ni mengi zaidi kuliko maoni ya pamoja. Kufanya majadiliano na mazungumzo kuhusu masuala yanayosababisha mgongano ni msingi wa kuboresha uhusiano kati ya nchi mbili.
Kuhusu mgogoro wa Syria, Ryabkov amesisitiza kuwa, Marekani haijatoa shinikizo la kutosha kwa makundi ya upinzani ya Syria, ili yasitoe sharti la kuhudhuria mkutano wa Geneva. Russia ina maoni tofauti kuhusu kualikwa kwa Iran kwenye mkutano huo, na inaona mkutano huo hautapata mafanikio bila ya ushiriki wa Iran