24 Agosti 2013 - 19:30
Iran yaionya Marekani dhidi ya Syria

Iran imeionya Marekani dhidi ya kuvuka mipaka kuhusu suala la Syria. Shirika la habari la Syria limemnukuu kamanda mkuu wa jeshi la Iran Masoud Jazayeri, akisema Marekani inaelewa wazi kuwa haiwezi kuvuka mipaka kuhusu suala la Syria na endapo itafanya hivyo basi itajutia uamuzi wake.

Ripoti ya ABNA- Tamko hilo la Jazayeri linakuja muda mfupi tu baada ya makamanda wa Marekani kutoa taarifa kuhusu uwezekano wa kufanya uingiliaji wa kijeshi nchini Syria kutokana na madai kuwa serikali ya nchi hiyo ilitumia silaha za kemikali dhidi ya raia. Hata hivyo serikali ya Syria imekanusha madai hayo.