24 Agosti 2013 - 19:30
Dr.Ruhali kumpokea rasmi mfalme wa Omani

Rais wa Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran leo adhuhuri alimpokea rasmi mfalme wa Omani katika mji mkuu wa Tehran.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Hujatul Islam walmuslimin Dr.Hasan Ruhani rais wa Jamuhuri ya Kiislamu wa Iran leo adhuhuri alimpokea rasmi Sultan Qabus mfalme wa Omani katika mji mkuu wa Tehran.

Katika mapokezi rasmi hayo kulisomwa nyimbo za nchi mbili hizo kisha kupelekwa sehemu husika.

Safari hii inalenga kuimarisha uhusiano mzuri wa nchi mbili hizo na ujirani wema na kusaini baadhi ya mikataba.