Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Wiki mbili zilopita vyombo vilivyokaribu na waasi vilieleza kuwa Sheikh Badr Ghazal aliuwawa na waasi wa nchi wa Syria wanaojiita waokozi wa za kiislamu (Iraq na Sham).

Sheikh huyo alitekwa na waasi wa Syria wiki mbili zilopita na kusambaza picha zake baada ya kupigwa vibaya na waasi hao huku alionekena kuvuja damu kwa kipigo kikali.

Siku kadhaa zilopita zimesambazwa picha kuthibitisha kuwa Sheikh huyo kaishauwawa na waasi hao, na picha hizi ni ushahidi tosha wa kuonyesha unyama wa watu hao ambao wadai ni wasuluhishaji.

Waasi wa Syria wadi sasa wameshindwa katika vita na wameona njia ya kulipiza kisasi ni kuteka wanazuoni, na hiki si kitendo cha kwanza cha waasi hao Syria wanasivi nzuri ya kuuwa wananchi na wanazuoni bila sababu yoyote ile ya msingi.