Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Marekani baada ya jitihada muda mrefu kufeli katika uamuzi wake wa kuvamia Syria kijeshi, Uingereza ni moja kati ya nchi zilizokuwa zikiunga mkono Marekani imejitowa katika fikra za kuvamia Syria baada ya Bunge la nchi hiyo kukataa kuingilia na kuvamia Syri kijeshi na kutaka kutafuta njia mbadala ambayo ni kidiplomasia.
Baada ya uamuzi huo nchi nyingi zilishuhudia maandamno makubwa na mamia ya watu kuandamana dhidi ya vita ya Syria, Uingereza waliandama wananchi kupinga kuingilia nchi yao katika mambo ya Syria.
Marekani nako kulishuhudia maandamano makubwa ya kupnga nchi yao kuvamia Syria kivita kwa madai ya kutumia serikali ya Syria silaha za kemikali dhidi ya wananchi wake, na kueleza hiyo ni njia nyengine ya kutaka kuharibu hali ya usalam nchini Syria kama walivyofanya Iraq kwa madai ya kuwa serikali ya Iraq ni silaha za Nyuklia.
Uturuki nako mamia ya wananchi waliandamana kwenye kambi ya jeshi ilokuwepo mpakani mwa Syria na Uturuki kuitaka nchi yao kutotumia ardhi ya dhidi ya Syria na kuitaka nchi kujiepusha mbali na fitina hizo za Marekani.
Mazayuni walivyokuwa na uwoga juzi walitangaza kuwa mnamo siku ya Alkhamisi (ilopita) Marekani ndio imepangilia kuvamia Syria, na kutangazi wananchi wa Israel kuchukua mask za Nyuklia kama ikitokea vita Syria itavamia Israel kwa silaha za kemikali.
La ajabu ni kwamba uamuzi wa kuvamia Syria Umoja wa Mataifa umepinga vikali kutokana na kutopatikana na ushahidi matumizi ya silaha za kemikali, na kueleza madai ya Marekani hayana nafasi kwani kila sehemu ilotumiwa silaha ya kemikali athari zake hubaki hadi wiki mbili, kwa matiki hii madai ya Marekani kuwa serikali ya Syria ilichelewa kuruhusu wakaguzi wa Umoja wa Mataifa sio kweli waliruhusiwa ndani ya muda muafaka.