Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Hitilafu na mzozo mkali baina ya vikundi vya waasi kupamba moto kutokana na kila kikundi kupangilia ratiba ilokuwa dhidi ya wengine.
Televisheni ya Sky News ilieleza kwamba: Huku Mashariki na Kaskazini mwa Syria kukishuhudia mapambano makali baina ya vikundi viwili vya waasi, kikundi cha waokozi wa Iraq na Sham(Syria) kueleza kuwa wamekata uhusiano na misada yote walokuwa wakisaidia kikundi cha waasi Al-Nasr Syria kutokana na mvutano na hitilafu walokuwa nazo baina yao na kikundi hicho cha Al-Qaida.
Sky News: Kikundi cha waokozi wa Iraq na Sham(Syria) ni kikundi pekee kilokuwa kikiwasaidia waasi wa Al-Nasr Syria kwa kuwa kikundi hicho(Kikundi cha waokozi wa Iraq na Sham(Syria)) kuna baadhi ya sehemu zipo mikononi mwao na kutumia mali asili kwa kuwasaidia Al-Nasr.
Kikundi cha Al-Nasr ambacho wapiganaji wake wengi ni watuwa nchi tofauti hapo kapla waliomba Kikundi cha waokozi wa Iraq na Sham(Syria) kujiunga na kikundi hicho na kuunga vikundi vingine kama Al-Sham, Al-Tauhid na Al-Islam kwa lengo la kuvunja Jeshi Huru la Syria, kulingana na habari hii wengi walikuwa wakitambua kuwa kikundi cha waasi Al-Nasr ndio waogozaji wakuu, wapiganaji na wapinzani wakuu wa serikali ya Syria.