29 Oktoba 2013 - 20:30
Kada wa Muslim Brotherhood Misri akamatwa

Serikali ya misri imefanikiwa kumtia mikononi mwanasiasa maarufu Essam El Arian ambaye pia alikuwa ni kada wa Muslim Brotherhood na Makamu Mwenyekiti wa chama chaJustice and Freedom ambacho pia ni tawi la Muslim Brotherhood.

Awali mwendesha mashtaka wa Misri hiyo aliagiza Essam El Arian akamatwe tangu mwezi Julai baada ya Rais Mohammad Morsi ambaye pia alikuwa ni mwanachama wa Justice and Freedom kuondolewa madarakani.

inasadikiwa kuwa Kukamatwa kwa kada huyo ni moja ya hatua ya serikali iliyopo madarakani kudhibiti hatakati zinazoendeshwa na kundi hilo lenye itikadi kali za kiislamu

 .