Kuolewa Ummu Kulthum na Omar(RA) kwa upande wa Mashia waelezwa kwa mfumo kama ufuatao:
Kuolewa Ummu Kulthum na Omar(RA) ni suala la kisiasa ambalo Omar(RA) alitumia ili kufumba macho suala la Ukhalifa(Uongozi baada ya Mtume) na kulazimisha Ally akubali kumuoza Ummu Kulthum na Ally akamuakilisha ndugu yake Abbas kuwa msimamizi wa ndoa hiyo, Ummu Kulthum alifariki kabla ya Omar(RA) na Omar(RA) hakuweza hata siku moja kukutakana na Ummu Kulthum kutokana alikuwa na umri mdogo... na suala kuwa na mtoto upande wa Shia limekanushwa na kupingwa kutokana na riwaya.
Madai ya kusema imekuwaje ally(AS) amuozeshe mtoto wake kwa Omar(RA) ilihali ya kuwa Omar(RA) ni kafiri?!! Jibu lake ni kwamba; Ally(AS) kumuoza mtoto wake kwa Omar(RA) si kinyume na Isma la hasha kwani kuna manabii waloowa wake wasokuwa wema kama Nabii Nuh(AS) na Lut(AS) sembuse Ally(AS) ambaye si Nabii, pia kuozeshwa Omar(RA) haimaanisha kuwa Ally(AS) hana ugomvi na Omar la hasha Hadith zaeleza kuwa Omar(RA) alilazimisha kuowa ndio maana Ally(AS) alilazimika kumuoza Omar(RA).
3-Madai, kukanusha ugomvi baina ya Bi Fatima(AS) na Omar(RA) na Abubakar(RA) ni kitu kilichokuwa wazi kihistoria... Swali; kama kweli kulikuwa hakuna matatizo baina ya Bi Fatima(AS) na Omar na Abubakar, kwanini leo kaburi la Bi Fatima(AS) halifahamiki sehemu lilipo?! ilihali ya kuwa yeye alifariki baada ya miezi sita ya kifo cha Baba yake Mtume(S.A.W.W)!!, aidha ushahidi tunao kuwa Bi Fatima(AS) alifariki akiwa na ghadhabu kali kunako mambo walofanya Abubakar na Omar... ushahidi wa maneno ni; SAHIH BUKHARI, JUZ 3, UK 1126, HADITH 2926. SAHIH BUKHARI, JUZ 4, UK 1549, HADITH 3998. SAHIH BUKHARI, JUZ 6, UK 2474, HADITH 6346.
4-Madai ya kutowa baiya Ally(AS) kwa Abubakar sio SAHIHI kutokana na ushahidi wa Hadith kuwa Ally(AS) na Banii Hashim baada ya kufariki Bi Fatima(AS) hawakutowa baiya.. KITABBU cha IHQAQUL HAQ, JUZ 1, UK 121....Kwanini twashadidia(twakazania) kusema baiya ya Ally kwa Abubakar tu, kusahau kwamba baada ya kufariki Mtume(S.A.W.W) Abubakari na Omar hawakushiriki katika mazishi ya Mtukufu Mtume(S.A.W.W)!!! kwanini suala hilo pia lisizungumziwe hadharani watu walijuwe?!! Kwa madai ya kuwa Abubakari na Omar walikuwa ni watu wa karibu ya Mtume(S.A.W.W) je! Ukaribu ni kipindi cha uhai wa Mtume tu?!
5-Ukafiri wa Muawiya hakuna shaka ndani yake, Waislamu wote wakubaliana kuwa Mtume alimuombea dua mbaya Muawiya baada ya Mtume alivyomwita Muawiya akamjibu mwambieni ninakula Mtume(S.A.W.W) alisema: ALLAH ASISHIBISHE TUMBO LAKE. Baiya ya HASAN(AS) kwa MUAWIYA ilikuwa ni mkataba wasuluhu wa kisiasa walokubaliana kua MUAWIYA akifariki kabla ya HASAN(AS) uongozi utarejea kwa HASAN(AS), na kama HASAN(AS) atafariki kabla ya MUAWIYA basi uongozi utakwenda kwa HUSEIN(AS) baada ya MUAWIYA...Kutokana na kwenda kinyume na suluhu na mkataba huo, MUAWIYA alifanya njama za kumuuwa HASAN(AS) ili utawala na uongozi amkabidhi YAZID(alolaaniwa na allah) mtoto wake, kwa hilo MUAWIYA alifaanikisha kumuuwa HASAN(AS) na utawala na uongozi akampa mtoto wake YAZID na ndio maana HUSEIN(AS) hakukubaliana na hayo alikuwa dhidi ya YAZID kwa kuwa YAZID alikuwa ni MUOVU, FASIQ NA KAFIRI kama Baba yake, Hatimae YAZID(laana za Allah ziwe juu yake) alimuuwa HUSEIN(AS) mjukuu kipenzi wa Mtume(S.A.W.W).
6-Ally(AS) kuwa na watoto wenye majina kama ABUBAKAR, OMAR na UTHMAN, Tunajibu kama ifuatavyo;
1-Mtoto wa Ally(AS) mwenye jina la Abubakar, Abubakar halikuwa jina lake bali ni KUNIA yake jina lake lilikuwa ni MUHAMMAD ASGHAR... na KUNIA hiyo haikuwa ABUBAKAR tu bali alikuwa na KUNIA nyingine ya UBAIDULLAH..rejea KITABU MUUJAM RIJALUL HADITH, JUZ 12, UK 88.
2-Mtoto wa Ally aitwae Omar sio Ally alimwita Omar bali Omar mwenyewe ndiye alimwita Omar kutokana na mtoto huyo alizaliwa siku alozaliwa Omar...rejea KITABU SIRAT AALAMU NUBALAA, JUZ 4, UK 134.
3-Mtoto wa Ally(AS) kuitwa UTHMAN sio UTHMAN IBN AFAAN KHALIFA WA TATU la hasha jina hilo ni jina la ndugu yake alikiitwa UTHMAN IBN MADH-UN na ndio maana akaitwa UTHMAN...rejea KITABU MAQATILU TALIBIN, JUZ 1,UK 23.
7-Ally(AS) kukalia kimya UKHALIFA wa ABUBAKAR si maana kuwa Ally(AS) alikuwa atambuwi kuwa yeye ni kiongozi kutoka moja kwa moja kwa Mtume(S.A.W.W) bali alikaa kimya kwa kuhifadhi maslahi ya Uislamu...rejea VITABU, MUSNAD ABII DAUD, JUZ 4,UK 470, HADITH 2875. MUSTADRAK ALAA SAHIHAIN, JUZ 3, UK 134. Ushadi ni mwingi wa kuthibitisha uongozi wa Ally(AS).
8-Ghaiba ya Imam wa kumi na mbili si kwa Mashia tu na Imam wa kumi na mbili si wa Mashia tu ni wa Waislamu wote, ushahidi rejea VITABU, SAHIH BUKHAR NA SAHIH MUSLIM MLANGO WA KUSHUKA NABII ISSA(AS).
HUU NI MUHTASARI WA MAJIBU WA VIPEPERUSHI VILIVYOSAMBAZWA NA WATU WASOTAMBUA USHIA, KILA SUALA LILOZUNGUMZIWA KATIKA VIPEPERUSHI HIVYO MENGI NI MADAI TU YASOKUWA NA DALILI, KAMA KUONGELEA QURAN YA IMAM ALLY(AS) ILIKUWA KAMA TAFSIRI YA QURAN ALIANDIKA NA KUPANGILIA KILA SURA NA AYA KUTOKANA NA MUDA ILOSHUKA AYA NA SURA, QURAN YA LEO NI RIWAYA HAFSI KUTOKA KWA AASIM NA NI QIRAA NA SI ILE QURAN YA IMAM ALLY(AS), KWA HIYO MADAI HAYO HAYANA NAFASI KWANI NI MADA MBILI TOFAUTI KWA WABOBEZI WA ELIMU YA ULUMIL QURAN.
KWA MANTIKI HII KWA KILA ATAKAETAKA ZUNGUMZIA MASUALA KAMA HAYA LAZIMA AWE AMEJITOSHELEZA KIELIMU KUONGEA VITU BILA USHAHIDI WOWOTE ULE.