3 Desemba 2013 - 20:30
Mashahidi ambao katika kuzikwa watabasamu

Shahid Sayyid Wasam almaarufu kama Sayyid Nasrullah aliuwawa Damaskas Alkhamis ilopita alipokuwa akihami Haram ya Bibi Zainab(as), alishuhudiwa akitabasamu baada ya Shahada yake, pia Shahid Ally Mu`umin kijana wa Bahrain alishuhudiwa katika hali hiyo hiyo, na wengineo km Habib Lakzai, Ridha Qambari, Muhammad Ridha Haqiqi na Hasan Taqi Golsefidi.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Somo la Shahada ya Imam Husein(AS) imekuwa wazi kwa kila mtu, somo hilo limeonekana katika mashahidi huku wakizikwa wakitabazamu.

1-Shahid Hasan Taqi Golsefidi

Wosia wa Shahid ; Ninafuraha sana pale ambapo watu watakuwa wakinikumbuka huku wakiimba Nauha na nyimbo za maombolezo ya Imam Husein(AS) na kumlilia Imam Husein, someni Nauha za Imam Husein(AS) mpaka umma na watu waamke kupitia Imam Husein(AS), pia nina siku kumi na mbili na daiwa naomba mnisaidie kufunga siku hizo,aidha sala ninazo nyingi naomba mnisaidie kulipa sala hizo, mali sina na kama nitakuwa nazo basi zitolewe kwanjia ya Allah ili niende kukutana Allah nimetanguliza chochote.

2- Muhammad Ridha Haqiqi

Huyu ni mmoja katika mashahidi na watetezi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

3- Ridha Qambari

Aidha huyu ni mmoja wa watetezi wa Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran katika vita ya miaka 8 na Sadam Husein.

4- Ally Mu`umin

Huyu ni muhandisi wa nchi ya Bahrain, aliuwawa na vikosi vya usalama vya Bahrain katika Maidan ya Luuluu.

5- Habib Lakzai

Huyu ni watetezi Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran, kauwawa katika Mkoa wa Ahwaz.

6- Sayyid Wasam Sharafu Din

Shahid Sayyid Wasam almaarufu kama  Sayyid Nasrullah aliuwawa Damaskas Alkhamis ilopita alipokuwa akihami Haram ya Bibi Zainab(as), alishuhudiwa akitabasamu baada ya Shahada yake.

Watu hawa ndio wanaojua maana ya Shahada na mtu kujitolea kwa ajili ya Allah huku nyuso zao zikionyesha bashasha na tabasamu kufurahia kile walichokifanya na kukitanguza mbele ya Mwenyezi Mungu.