31 Januari 2014 - 20:30
Kesi ya Morsi yaendelea

Aliyekuwa Rais wa Misri Mohammed Morsi amefikishwa mahakamani kwa mara nyingine kujibu tuhuma zinazomkabili.

Bwana Morsi na washirika wake 14 kutoka Muslim Brotherhood wameshtakiwa kwa kosa la kuchochea mauaji ya waandamanaji nje ya ikulu ya Rais mnamo mwaka 2012.
Morsi aliwasili mahakamani mjini Cairo kwa kwa helikopta ya jeshi kutoka gereza anakozuiliwa mjini Alexandria.
Wakati wa kusikizwa kwa kesi yake siku nne zilizopita ,bwana Morsi alipuuzilia mbali mashtaka dhidi yake na kukana uhalali wa mahakama huku akisema kuwa bado yeye ndiye rais halali wa taifa hilo aliyechaguliwa na raia.
Aling'atuliwa mamlakani na jeshi mnamo mwezi Julai mwaka uliopita baada ya kundi kubwa la raia kumkana.