Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa kosa la ufisadi wa mali za taifa na mauji yaliofanyika dhidi ya waandamanaji katika kipindi cha mapinduzi ya serikali iliopita yaliotokea mwaka 2011 nchini humo nakupelekea kupinduliwa utawala wa Gaddafi.
Watuhumiwa hao walisema kuiambia mahakama kuwa wao hawna uwezo wa kuwasiliana na mawakili wao kitu ambacho kiliwafanya wafike mahakamani hapo bila ya wakili wao, ambapo Abdallah Sanusiy alisema kuwa : nataka niwe kama wafungwa wengine na nipewe haki ya kukutana na ndungu zangu pia wakili wa kunitetea.
Wanashiria wa mahakama ya Libya wamesema kuwa tunatoa ruhusa kwa Sanusiy kuonana na ndugu zake, ama suala lakusema mawakili wao wamezuiliwa kukutana na watuhumiwa hao ni suala lisilokuwa sahihi.
Kikao hicho cha kuhukumiwa watuhumiwa hao kimefanyika baada ya siku moja ya kujiuzulu (Abdallah Thaniy) ambaye alikuwa waziri mkuu wamuda wa nchini hiyo, ambapo waziri huyo alichukuwa maamuzi hayo baada ya kuvamiwa yeye na familia yake na watu wasio fahamika.
Mahakama ya kimataifa na jumuiya zingine za haki za binadamu wamedhihirisha khofu zao katika suala zema la kuwatedea haki watuhumiwa hao katika mahakama za Libya.
Baada ya kikao hiki, kikao kijacho kitafanyika 27/4/2014 kwakuwa wahakiki wa faili hilo wanahitaji muda zaidi ili kukamilisha faili hilo.
Ama Sababu zilizo pelekea kufanyika kikao cha hukumu hiyo gerezani ni khofu ya kutokea furugu na gasia ndani ya mji mkuu huo, pia kipindi kilichukuwa kikifanyika kikao hicho kulikuwa na ulinzi mkali katika maeneo ya gereza hilo.
Kwamujibu wa ripoti hii Saad Gaddafi ambaye anafahamika kuwa ni mtu wa starehe kuwa mwanzoni mwa machi mwaka huu alirudishwa nchini Libya kutoka nchini Niger.
Watoto hao wawili wa Gaddafi pamoja na tuhuma zilizo tajwa hapo juu pia wanatuhumiwa kuchakachua bajeti ya taifa nakutumia pesa hizo katika masuala yao binafsi
Rejea:Irna