Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Husain Amir Abdul Ilahiyan msaidizi wa waziri wa mambo ya nje ya Iran ukanda wa Afrika alionana na Rais mpya wa jamhuri ya Misri (Abdul Fattahu Assisiy) nakumfikia ujumbe wa pongezi za Rais wajamhuri ya kiislamu ya Iran DK Hasan Ruhaniy nchini Misri kwa Rais huyo mpya.
Muakilishi huyo wa Iran alipokuwa akiwasili nchini Iran kutoka katika sherehe hizo za kiapo cha Rais mpya wa Misri alisema; nilipokutana na Rais huyo alionyesha utayari yeye na na wananchi wake katika kukuza fungamano na Jamhuri ya kiislamu ya Iran katika nyaja mbali kitamaduni na maendeleo.
Mwakilishi huyo wa masuala ya Afrika aliongeza kusema kuwa: tumepokelewa vizuri sana na Rais wa nchi hiyo naye alimtaka mwakilishi kumfikishia shukurani zake za dhati kwa Rais wa jamhuri ya Iran kwa kuitika wito na kuhudhuria katika shere hizo za kuapishwa na kuiombea mema serekali ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran kimaedeleo.
Katika safari hiyo mwakilishi huyo baada yakumaliza sherehe hizo alionana na Amiri Sulaiman ambaye ni walii Ahadi wa ufalme wa Saudi Aarabia nakuzungumzia masuala ya amani ya mashariki ya kati, katika mazungumzo yayo waligusia kuwa baina ya Tehran na Riyadh suala muhimu baina ya pande mbili hizo ni kuobeana amani na uthabiti katika kuijenga mashariki ya kati na maendeleo katika sekta mbali mbali pia kuitakia amani mashariki ya kati.
Pia katika safari yake hiyo alionana na Amiri Abdil Azizi naibu wa waziri wa mambo ya nje ya Saudia kisha kuzungumzia safari ya waziri wa mambo ya nje ya Iran nchini Sudia nakusisitiza kuwa wako katika kuandaa kupokea ugeni wa waziri huyo wa mambo ya nje ya Iran katika masiku yajayo.
10 Juni 2014 - 21:43
Msimbo wa Habari: 615107
Rais wa jamhuri ya Misri alipokea ugeni wa naibu waziri wa mambo ya nje ya Iran (anae husika na masuala ya Afrika) aliyekuwa amemuakilisha Rais wa Iran katika sherehe hizo, mwakilishi huyo alifikisha ujumbe na pongezi za Rais wa Iran kuhusu ushindi wa Rais mpya wa Misri