20 Juni 2014 - 16:09
Mfalme wa Saudi Arabia aonana na Rais wa Misri mjini Cairo

Mfalme wa Saudi Arabia kwa mara ya kwanza kusafiria mjini Cairo baada ya kupinduliwa Husni Mubarak mwaka 2011 ambapo katika safari yake hiyo ataonana na Rais mpya wa nchi hiyo Abdul Fattah Alsysy mjini Cairo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA:  vyanzo vya kisiasa na ulinzi  nchini Misri vimetoa taarifa kwa vyombo vya habari vya ufaransa kuwa: mfalme Abdallah wa Saudi Arabia siku ya ijumaa atauonana na Rais wa nchi hiyo mjini Cairo ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kupinduliwa utawala wa dikteta wazamani wa nchiyo Husni Mubaraka mwaka 2011.
Saudi Arabia iliafikiana na kitendo cha kutolewa madarakani kwa Muhammad Mursiy kupitia Alsysy ambaye alikuwa kamanda mkuu wa Misri katika kipindi cha utawala wa Mursiy, nasaudia baada ya mapinduzi hayo ya kijeshi aliutoa tamko la msaada wa mabilioni ya Dola kwaserikali ya nchi hiyo.
Mkuu wa ubalozi wa Saudi Arabia nchi Cairo siku ya alhamisi aliwaambia waandishi wa habari wa ufaransa kuwa: mfalme wa Saudi Arabia atakuwa na mapumziko mafupi mjini Cairo ambapo ataonana rasmi na Rais wa nchi hiyo, aidha inatarajiwa kuwa Rais wa Misri ataenda kumpokea mgeni wake katika uawanja wa ndege wakimataifa mjini Cairo.
Mmoja kati ya wasimamizi wa masuala ya ulinzi katika uawanja wa ndege wa Cairo amesisistiza habari hizo zilizoenea kuhusu kukutana mfalme wa Saudi Arabia na Rais wa nchi hiyo nakusema vyombo vya ulinzi viko katika hali yakuanda mazingi na hali ya ulinzi katika uawanja wa ndege huo kwaajili ya kuonana viongozi hao.
Baada ya kutolewa madarakani Rais Muhammad Mursiy Riyadh ilitoa kauli ya kutoa msaada wa Euro bilioni tano pia Qatar , Kuwait na Emirate hatimae kufika kiwawango cha Dola bilioni saba