15 Julai 2014 - 05:17
Hamas yakataa kusimamisha vita

Kikundi cha wanamgambo wa kiparestina Hamas kimekataa kata kata ombi la Misri la kusimamisha vita.

mzungumzaji wa Hamas bwana Fawzu Barhum amesema kwamba: "Hatukubali kusimamisha vita, kabla ya kufikia muafaka wa makubaliano,kwani katika vita huwa haisimamishwi vita kisha kufanya makubaliano, bali hufanywa makubaliano kisha husimamishwa vita".

Israel inaendeleza mashambulizi makali huko ukanda wa Gaza, kwa siku saba mutawaliya, katika mashambulizi hayo watu wasio pungua 190 wamepoteza maisha na zaidi ya 1,280 wamejeruhiwa.
Mashambulizi ya Israel yalianza tarehe 8 Julai.