4 Oktoba 2014 - 17:35
Daesh wamuua msamalia mwema kutoka Uingereza/Picha

Kundi la kigaidi la Daesh limemchinja msamalia mwema kutoka kwa Uingereza.


Kundi la kigaidi la Daesh limemchinja msamalia mwema kutoka kwa Uingereza.
Henning mwenye umri wa miaka 47 ambaye ni dereva wa texi kutoka kaskazini mwa Uingereza alitekwa nyara mwezi Disemba mwaka uliopita alipokuwa akilifanyia kazi shirika moja la kutoa huduma za misaada kwa wakimbizi nchini Syria.
Kundi hili la kigaidi la Daesh ambalo limejikita na kudhibiti maeneo ya mpakani mwa Syria na Iraq tayari lishawaua waandishi wa habari ambao ni raia wa Marekani James Foley na Steven Sotlof pamoja na mfanyikazi wa kutoa huduma za misaada kutoka Scotland David Haines.
Daesh wamekuwa wakifanya jinai na unyama wa hali ya juu kwa raia wa Syria tangu mwaka 2011, wamekuwa wakidhulumu, wakibaka na kuchinja watu hadharani.