Kiongozi Muadhamu wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran katika hafla ya sherehe za Eid Ghadir amesema kuwa Marekani na washirika wake hawapo kupambana na Magaidi wa Daesh bali kuchochea tofauti kati ya waislamu.
Aliongeza kwa kusema kuwa,Marekani na washirika wake wakishirikiana Uingereza ambayo ndio stadi wa kuanzisha na kusambaza chuki na fitna ndio walio asisi na kuanzisha makundi ya kigaidi ya Al-Qaeda na Daesh kwa lengo la kukuza tofauti kati ya waislamu na kukabiliana na Jamhuri ya kiislamu la Iran lakini kwa bahati mbaya makundi haya yanawashambulia mpaka waasisi wake.
Kiongozi huyu Muadhamu ambaye pia ni amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya Iran, amesema kuwa lengo kubwa la Marekani na washirika wake ni kuleta tofauti kati ya madhehebu mawili makubwa katika uislamu, dhehebu la Shia na Sunni.
Ameendelea kusema kuwa lengo lingine la maadui wa uislamu ni kutenganisha uhusiano wa dini ya kiislamu na masuala ya kisiasa na kuhakikisha kwamba dini inakuwa ni jambo la ziada katika maisha na halitakiwi kujihusisha katika mambo ya kijamii.
Kiongozi huyu Muadhamu amesema kuwa tukio la Ghadir Khum na historia ya uislamu ni ishara tosha kwamba dini ya kiislamu haiwezekani kutenganishwa na siasa.
Sayid Ali Khamenei ameendelea akisema kuwa tukio la Ghadir Khum ndiyo asasi na msingi mkuu wa fikra za dhehebu tukufu la Shia na kwamba historia ya tukio la Ghadir haitakiwi kufumbiwa macho wala kusahauliwa, kwani ina faida nyingi katika uhai wa uislamu.
Kiongozi huyu pia amesisitiza umuhimu wa waislamu kuungana na kuondoa tofauti zao zinazokuzwa na maadui wa uislamu.
Yafaa kuashiria kwamba: Tukio la Ghadir ni tukio lililotokea mwaka wa 10 hijiria, tukio hili lilitokea katika safari ya mwisho ya hija ya mtume Muhammad s.a.w ambapo aliwaaga waislamu kwamba hataonana nao tena na kwamba anamuacha Ali bin Abitwalib kuwa ni kiongozi wa uislamu baada yake, siku hii pia ni siku ambayo dini ya tukufu ya kiislamu ilitimia, na maadui wa uislamu walikata tamaa ya kuuharibu uislamu kwani maadui wa uislamu walidhani kwamba kifo cha mtume ndio itakuwa mwisho wa uislamu, lakini kinyume na matarajio yao, mtume anamuweka madarakani Ali bin Abi Twalib kama kiongozi wa uislamu atakaye endeleza misingi na itikadi za mtume Muhammad s.a.w.
13 Oktoba 2014 - 16:55
News ID: 644118

Kiongozi Muadhamu wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran katika hafla ya sherehe za Eid Ghadir amesema kuwa Marekani na washirika wake hawapo kupambana na Magaidi wa Daesh bali kuchochea tofauti kati ya waislamu.