Kiongozi wa kidini ambaye pia ni kiongozi serikalini Ayatollah Jannatii katika kikao hicho cha kimaitaifa amesema kuwa: inatupasa kutumia kila njia kuwafahamisha watu ukweli kuhusu magaidi na wote wenye misimamo mikali wanayoinasibisha na uislamu, kuwa vitendo vyao na misimamo yao haihusiani na uislamu.
Ayatollah Jannatii: ameendelea kusisitiza umoja wa madhehebu ya kiislamu na kwamba waislamu wote wawekitu kimoja na wapambane na maadui wa uislamu wanaotaka kuleta fitina na uhasama katika dini tukufu ya uislamu.
Ayatollah Jannatii: amesisitiza kuwa matukio ya Takfir na waislamu wanaofanya ukatili, ugaidi na jinai kwa jina la kiislamu ni masuala ya kisiasa, yenye malengo ya kuchafua dini tukufu ya uislamu.
Ameongeza kusema kuwa: wanasiasa na mabepari wa dunia wamehisi hatari baada ya kuona muamko wa waislamu, hivyo wakaamua kutengeneza vikundi vinavyodani kuwa ni vya kiislamu, vifanye jinai na mauaji ili kuchafua mtazamo wa watu kuhusu dini tukufu ya uislamu.
Amendelea kusema kuwa: Vijana na waislamu msihadaike na mawaidha na wito wa jihadi unaofanywa na makundi haya ya kigaidi, watu hawa hawahusiani na uislamu, na wanachokifanya ni tofauti kabisa na jihadi ya kiislamu, jihadi ya kiislamu si mauaji wala dhuluma wala ubakaji.
Katika Kongamano hilo mwenyeji wa kongamano Ayatollah Makarim Shiraz, baada ya ufunguzi wa kongamano alisema kuwaambia wanazuoni waliohudhuria katika kongamano hili kuwa: Tutaa kimya mpaka lini na kutazama watu wakifanya jinai na mauaji kwa kutumia jina la dini ya kiislamu?
Aliendelea kusema kuwa ni wadhifa wa kila mwanazuoni kuhakikisha anapambana na fikra potofu za waislamu wenye siasa kali wanaofanya mauaji na kuyanasibisha na dini tukufu ya Amani.
Aliendelea kusema kuwa lengo kuu la kongamano hili ni kuufahamisha ulimwengu kuwa matukio yanayofanya na waislamu wa siasa kali, Takfir, Daesh na magaidi wote hayana uhusiano na dini tukufu ya kiislamu.
Alisisitiza kuwa kikundi cha Daesh ambacho maana yake ni Dola ya kiislamu ya Iraq na Sham, Si dola wala si cha kiislamu, watu wanatakiwa wafahamu jambo hili.
Dk: Alizadeh Musawi, ambaye ni msimamizi wa maandalizi ya kongamano hili amesema kuwa: katika kuchagua wanazuoni watakao hudhuria katika kongamanoi hili tumezingatia vigezo vitatu, kwanza: awe anapinga jinai za takfiri na wenye misimamo ya kuchupa mipaka, pili awe anaunga mkono na kupenda umoja wa madhehebu ya kiislamu uwepo, na tatu awe na mtazamo kuhusiana na jinsi ya kukabiliana na wanachafuzi wa dini tukufu ya kiislamu.
Dk: Alizadeh Musawi aliashiria kuwa: hapo awali tuliweza kupata wanazuoni elfu mbili (2000) wenye vigezo hivi duniani kote na katika hao elifu mbili, tukachagua wanazuoni mianne na ishirini (420).
Kongamano hili linafanyika katika Jamhuri ya kiislamu ya Iran, mji wa Qum ambao unahesabika kuwa ni makao makuu ya kielimu ya dhehebu la kiislamu ya Shia, ikifuatiwa na Najaf ya Iraq, Qum kunavyo vikuu vingi vya kiislamu na wanafunzi kutoka dunian kote wanachukua elimu kutoka katika mji huo, ambao umejaa wanazuoni na wataalamu wa elimu mbalimbali hususan elimu za dini tukufu ya kiislamu, Pia Falsafa na Siasa na masomo mengine.