Shambulio lililofanywa na mtu aliyeyatolea mhanga maisha yake dhidi ya gari la ubalozi wa Uengereza mjini Kabul nchini Afghanistan limeangamiza maisha ya watu wasiopungua sita.
Raia mmoja wa Uengereza na wengine watano wa Afghanistan ni miongoni mwa wahanga-polisi ya Afghanistan na wizara ya mambo ya ndani ya Uengereza mjini London zimesema.Zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa.Shambulio hilo limetokea katika eneo la shughuli nyingi za usafiri katika mji mkuu wa Afghanistan-Kabul,mahala yanakokutikana majengo mengi ya kigeni na ya kijeshi.Shambulio la bomu limeutikisa mji mzima wa Kabul.kundi la kiislamu lenye itikadi kali la taliban,limetangaza kuhusika na shambulio hilo.
Mashambulizi ya Muhanga na yakuvizia yamekuwa ni matukio ya mara kwa mara yanayowakabili raia wa nchi za Ulaya na Marekani nchi Aghanstan, hii inatokana na kisasi na chuki ya baadhi ya waafghanstan dhini ya mataifa hayo, kutokana na kuvamia nchi yao.