Serikali ya Syria imesema kuwa ndege za kivita za Israel zimeshambulia maeno kadhaa ya mji mkuu wa nchi hiyo Damaskas.
Katika kinachoitwa kuwasaidia magaidi, ndege za kivita za jeshi la serikali ya Israel zimeshambulia maeneo pembezoni mwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Damaskas, pia ndege hizo za jeshi la Israel zimeshambulia kiwanja cha ndege kidogo kilichopo katika mji wa Dimas.
Mashudhuda wanaeleza kuwa takribani milipuko isiyopungua kumi ilirindima katika mji wa Dimas, mpaka sasa serikali ya Israel haijasema kitu kuhusu mashambulizi haya.
Inaripotiwa kuwa ndege za kivita za jeshi la Israel mara kwa mara zimekuwa zikushambulia maeneo ya Syria tangu kuanza vita ndani ya Syria mnamo mwaka 2011.
Serikali ya Syria inaishutumu Israel na mataifa ya magharibi kwa kuwasaidia magaidi wanaofanya jinai dhidi ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo ya kiarabu.
Serikali ya Syria imesema imekamata shehena kadhaa za silaha zilitongenezwa Israel ambazo zilikuwa zikipelekwa kwa magaidi hao wanaotaka kuangusha utawala wa Bashar al asad, pia imeishutumu Israel kwa kuwafundisha magaidi hao mafunzo ya kijeshi na kuwasaidia katika nyanja mbalimbali.
Yafaa kuashiria kuwa tangu mwaka 2011 wapiganaji na magaidi wanaopata msaada kutoka katoka Israel, Qatar, Uturuki,Saudia Arabia na mataifa ya magharibi walipelekwa Syria kwa minajili ya kuangusha serikali ya Bashar al asad lakini kutokana na uimara wa jeshi la Syria kwa ushirikano na Jeshi la Jamhuri ya kiislamu ya Iran na jeshi la Hizbollah wameweza kuvunja matajio ya wavamizi hao ambao walitangaza bayana kuwa watauangusha utawala wa Syria ndani ya muda usiopungua miezi sita.