18 Desemba 2014 - 18:25
Yuval Steinitz: Palestina inatangaza vita

Waziri wa usalama wa Israel Yuval Steinitz amesema leo kuwa mswada wa azimio uliowasilishwa kwa niaba ya Palestina katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni tangazo la vita

Waziri  wa usalama  wa  Israel  Yuval Steinitz  amesema  leo  kuwa mswada  wa  azimio  uliowasilishwa  kwa  niaba  ya  Palestina katika  baraza  la  Usalama  la  Umoja  wa  Mataifa  ni  tangazo  la vita. Waziri Steinitz  amesema  hiyo si  hatua  ya  amani , bali  ni hatua  ya vita  ambayo  Palestina  inaelekeza.

Waziri Steinitz  ameiambia  radio  ya  Israel,  iwapo  mamlaka  ya Palestina  itaendelea  kukandamiza  majadiliano  ya  amani  na kuelekea  katika  hatua  za  kipekee  za  kidiplomasia  dhidi  ya Israel , nchi  hiyo  itafikiria  fursa  zote, ikiwa  ni  pamoja  na  kuivunja mamlaka  hiyo.

Jordan , kwa  niaba  ya  wapalestina, imewasilisha  mswada  wa mwisho  jana, ambao  unatoa  wito  wa  makubaliano  ya  amani katika  muda  wa  mwaka  mmoja  baada  ya  mswada  huo kuidhinishwa  na  Israel  iondoe  majeshi  yake  kutoka  katika  ardhi inayoikalia  kabla  ya  mwisho  wa  mwaka  2017.

Israel inaogopa kufikishwa mswada huo, kwani hatua hiyo itapelekea Israel kuwa dhaifu, hivyo Israel na swahiba wake Marekani wanajaribu kila njia kuishawizi Palestina kwa ahadi za kitoto ili iachane na mpango huo, na kuiacha Israel iendelee kukalia ardhi za Palestina ilizozinyang’anya kwa nguvu.