Rais wa Cameroon Paul Biya amesema wanajeshi wa nchi hiyo wamemkomboa raia wa Ujerumani aliyekuwa akizuiliwa na kundi la itikadi kali za kiislamu la Boko Haram kwa miezi sita iliyopita. Katika taarifa yake iliyosomwa katika televisheni ya taifa, Biya alisema Mjerumani Robert Eberhard Nitsch alikombolewa katika operesheni maalumu iliyofanywa na jeshi la Cameroon na maafisa wa usalama wa nchi washirika. Rais Biya hakutoa maelezo ya kina kuhusu operesheni hiyo ya kijeshi na hakusema Mjerumani huyo alitekwa nyara katika mazingira gani mnamo mwezi Julai mwaka jana. Balozi wa Ujerumani nchini Cameroon, Klaus-Ludwig Keferstein, ameishukuru Cameroon kwa kumkomboa Nitsch ambaye atafanyiwa uchunguzi wa kiafya kabla kurejeshwa nyumbani Ujerumani.
22 Januari 2015 - 12:51
Msimbo wa Habari: 666425
alikombolewa katika operesheni maalumu iliyofanywa na jeshi la Cameroon na maafisa wa usalama wa nchi washirika