25 Januari 2015 - 10:55
Chama tawala chashinda uchaguzi Zambia

Mgombea urais wa chama tawala cha Patriotic Front Edgar Lungu ameshinda katika uchaguzi wa rais nchini Zambia dhidi ya mpinzani wake mkuu Hakainde Hichilema.

Mgombea urais wa chama tawala cha Patriotic Front Edgar Lungu ameshinda katika uchaguzi wa rais nchini Zambia dhidi ya mpinzani wake mkuu Hakainde Hichilema. Uchaguzi huo uliitishwa kufuatia kifo cha Rais Michael Sata aliyefariki dunia mwezi Oktoba mwaka jana baada ya kuugua. Tume ya uchaguzi nchini Zambia imetangaza Lungu amepata asilimia 48.3 ya kura huku Hichilema wa chama cha United Party for National Development akipata asilimia 46.7. Kaimu Jaji mkuu wa Zambia Lombe Chibesakunda amesema baada ya kura zote kuhesabiwa kutoka maeneo bunge 150, Lungu ameibuka mshindi. Lungu ambaye ni waziri wa sheria na ulinzi wa Zambia ataliongoza taifa hilo hadi mwaka ujao kukamilisha muhula uliosalia wa utawala wa Sata, na ameahidi kukamilisha miradi ya maendeleo na kiuchumi iliyoanzishwa na Sata.