30 Januari 2015 - 19:37
 Washia 35 wauwawa katika shambulizi la bomu Pakistan

Afisa mmoja wa polisi nchini Pakistan amesema idadi ya waliokufa katika mripuko wa bomu kwenye msikiti mmoja wa washia kusini mwa nchi hiyo imeongezeka na kuwa watu zaidi ya 35. Ripoti za awali zilisema waliouwawa ni watu 20.

Naibu  Inspekta wa polisi wa wilaya ya Shikarpur Sain Rakhio Mirani, amesema  maiti 31 zilipelekwa katika hospitali ya  wilaya hiyo. Televisheni ya Pakistan ilionyesha picha za wakaazi na waumini wa eneo hilo, wakisafirisha hospitali  maiti na majeruhi. Bado hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo, lakini  mara nyingi Waislamu wa  tikadi kali wa madhehebu ya Sunni wamekuwa wakizishambulia taasisi za kidini za Washia, wakidai si Waislamu wa kweli.