1 Februari 2015 - 13:07
Viongozi wa Afrika waitaka kesi dhidi ya Bashir na Ruto zisitishwe

Mahakama ya jinai ya kimaitafa imekuwa ikiwaandama viongozi wa Afrika na kuacha viongozi wa mabala mengine ambao wanatuhuma za jinai, uhalifu na mauaji kama rais wa Marekani wa zaman Joji Bush, waziri mkuu wa Uingereza Tony Brea na viongozi wa Israel ampo watu hawa wamefanya jinai zaidi hata ya zile walizoanya viongozi wa Afrika.

Viongozi wa Afrika wanasema korti kuu ya kimataifa ya uhalifu mjini The Hague,ICC ingepaswa kuachilia mbali au kuakhirisha kesi dhidi ya rais Omar Al Bashir wa Sudan na makamu wa rais wa Kenya William Ruto hadi madai yao kuhusu korti hiyo na mapendekezo ya kuufanyia marekebisho mkataba wa Roma yatakapozingatiwa.Matakwa hayo yametajwa katika ripoti iliyochapishwa na viongozi wa Afrika mwishoni mwa mkutano wao wa kilele mjini Addis Abeba.Umoja wa Afrika unaituhumu korti kuu ya kimataifa mjini The Hague kuwaandama zaidi waafrika.Mashirika ya haki za binaadam yanaukosoa Umoja wa Afrika kwa kudai kesi dhidi ya viongozi wa kiafrika zisitishwe na kufika hadi ya kusema Umoja huo unashajiisha watu kufanya makosa bila ya kuwajibishwa.