Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mmoja kati ya maprofesa wa viuo vikuu vya Marekani ameyasema hayo huku akisisitiza kuwa kuasisiwa kwa kikundi cha Daesh katika mashariki ya katika ni katika kutekeleza malengo ya ubepari na ubeberu wa nchi za kimagharibi.
Arthur Avfam amesema: kikundi cha kigaidi cha Daesh kimewekwa kwa lengo la kuwahofisha wasiokuwa Waislamu na kukuza chuki kwa Waislamu ulimwenguni, kikundi hicho kimeasisiwa na serikali ya Marekani na Israel ambapo kwa vitendo vyao vya kinyama wakitumia alama ya dini katika bendera yao ili kujenga mitazamo asi dhidi ya dini ya Kiislamu.
Naye aliendelea kusema kuwa lengo asili ya kuasisiwa kikundi hicho na vikundi vingine vinavyo shabihiana na hicho ni kukuza hisia ya uadui na hofu dhidi ya Waislamu na Uislamu ulimwenguni.
Ufafanuzi wa Profesa huyo wa viuo vikuu Marekani umepelekea baadhi ya makamanda wa Daesh nchini Pakistan kukiri kuwa hupewa pesa na vifaa vya kivita kutoka katika nchini Marekani na baadhi ya nchi za kimagharibi.
Kwamujibu wa ripoti hii ni kwamba serikali ya Marekani kabla ya kutokea vurugu za Syria ilikuwa ikitoa mafunzo ya kuandaa kikundi cha Daesh nchini Jordan.
7 Februari 2015 - 21:05
Msimbo wa Habari: 669785
Profesa wa viuo vikuu vya Marekani amesema: kuasisiwa kikundi cha kigaidi cha Daesh ni moja kati ya nyenzo za kuwatia hofu wasiokuwa Waislamu kuusambaratisha Uislamu kwakutumia alama ya dini katika bendera zao.