Uongozi wa Palestina unakutana wiki hii kwa mazungumzo muhimu kuhusiana na hali ya baadaye ya mamlaka ya Palestina , ambayo uhai wake uko hatarini baada ya Israel kuzuwia chanzo muhimu cha mapato.
Chama cha ukombozi wa palestina PLO , kinachotambulika kama mwakilishi halali wa watu wa Palestina pamoja na chombo chake kinachotoa maamuzi , vitajadili masuala kadhaa ya dharura ya kiuchumi na kisiasa.
Mkutano huo wa Ramallah unaoanza Jumatano utaangalia hali iliyopo ya dharura ya mzozo wa kifedha unaikabili mamlaka hiyo ya Palestina.
Katika muda wa miezi miwili iliyopita , Israel imezuwia mamia ya mamilioni ya dola kutokana na mapato ya kodi kwa mamlaka hiyo, baada ya hatua ya Palestina kujiunga na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ili kuishitaki Israel kwa madai ya uhalifu wa kivita.
Matatizo ya fedha yamesababisha mamlaka ya Palestina kushindwa kuwalipa wafanyakazi wake 180,000.
Israel ni ilichukua kwa nguvu ardhi za Palestina na kuwashambulia kwa silaha kali raia wa nchi hiyo na hatimaye kuwafanya kuwa dhaifu na kuwaacha katika hali ya umsikini wa hali ya juu.