Waziri wa zamani wa mambo ya nje, Hillary Clinton, amevunja ukimya wake juu ya utata uliozua mashaka kwenye kampeni yake ya kuwania urais. Mke huyo wa aliyekuwa rais wa Marekani, Bill Clinton, alijitokeza mbele ya waandishi wa habari hapo jana na kusema kwamba hakufanya jambo lisilo sahihi kwa kutumia akaunti yake binafsi ya barua-pepe kwa matumizi ya kiofisi wakati akiwa waziri wa mambo ya nje. Hillary Clinton anayewania uteuzi wa chama chake cha Democrat kugombea urais hapo mwakani, alisema matumizi hayo yaliruhusiwa na wizara na kwamba alidhani ingelikuwa rahisi kwake kutumia kifaa kimoja kwa barua za kazi na zake mwenyewe. Ingawa utata huo hadi sasa haujaathiri nafasi yake kama mgombea, umeathiri rikodi yake ya kuwa kiongozi mwenye tahadhari. Utetezi huo wa Hillary Clinton unaonekana kutopunguza juhudi za wabunge wa chama cha Republican kulitumia suala hilo kuimarisha uchunguzi wao juu ya vifo vya raia wanne wa Marekani kwenye ubalozi mdogo wa nchi hiyo mjini Benghazi, Libya, mwaka 2012.
11 Machi 2015 - 10:40
Msimbo wa Habari: 676071
Waziri wa zamani wa mambo ya nje, Hillary Clinton, amevunja ukimya wake juu ya utata uliozua mashaka kwenye kampeni yake ya kuwania urais.