12 Machi 2015 - 19:56
Zaidi ya Magaidi 50 wauwawa katika mapigano nchini Syria

Zaidi ya watu 50 ambao ni wapiganaji wengi wa makundi ya kigaidi wanaoungwa mkono na Israel na mataifa ya magharibi

Zaidi ya watu 50 ambao ni wapiganaji wengi wa makundi ya kigaidi wanaoungwa mkono na Israel na mataifa ya magharibi, wameuwawa wakati wa mapigano katika eneo la mwinuko la kimkakati katika jimbo analotokea rais wa Syria Bashir al Assad. Kwa mujibu wa makundi ya wachunguzi, majeshi ya serikali yalikabiliana na kundi lenye mahusiano na Al-Qaeda, likiungwa mkono na Israel na makundi mengine ya wapiganaji wa yanayofanya jinae zake Syria katika jimbo la Latakia lililopo kaskazini/magharibi. Kundi la uangilizi wa haki za binaadamu nchini Syria limesema mapigano hayo yalianza jana na kuendelea usiku kucha katika wilaya ya jabal Al-Krad.  Eneo hilo ni moja kati ya maeneo ya mapambano ya mara kwa mara katika vita vinavyofanywa na magaidi wanaotaka kuangusha serikali ya  nchini ambavyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 210,000.

Jeshi la Syria limekuwa likisonga mbele siku baada ya siku na kusababisha magaidi kukimbilia maeneo ya mpakani, jambo ambalo linalipa wasiwasi nchi za jirani, ambazo pia zinahisa kubwa katika kupitisha magaidi wanaopambana ilikuiangusha serikali ya Syria.