Siku tatu tu baada ya kusema anapinga ufumbuzi wa madola mawili wa mzozo wa Mashariki ya kati,waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amebadailisha msimamo wake."Hataki ufumbuzi wa taifa moja" amesema katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Marekani-NBC.Anataka ufumbuzi wa madola mawili utakaoleta amani ya kudumu.Jumatatu iliyopita,siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa Israel na katika juhudi za kuwazinduwa wapiga kura wa mrengo wa kulia,Benjamin Netanyahu alisema hakubaliani na fikra ya kuundwa dola ya Palastina.Hivi sasa yadhihirika,anabadilisha msimamo wake.
20 Machi 2015 - 11:30
Msimbo wa Habari: 677979
Siku tatu tu baada ya kusema anapinga ufumbuzi wa madola mawili wa mzozo wa Mashariki ya kati,waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amebadailisha msimamo wake."