22 Machi 2015 - 17:48
Uchaguzi wa mikoa nchini Ufaransa wafanyika leo

Wafaransa wanateremka vituoni katika mikoa yote ya nchi hiyo hii leo kuwachagua wawakilishi wao.Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia Front National,FN,kinachoongozwa na Marine Le Pen kinatazamiwa kuongoza matokeo ya uchaguzi huo

Wafaransa wanateremka vituoni katika mikoa yote ya nchi hiyo hii leo kuwachagua wawakilishi wao.Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia Front National,FN,kinachoongozwa na Marine Le Pen kinatazamiwa kuongoza matokeo ya uchaguzi huo.Tafiti za maoni ya wananchi ndio unaoashiria hali hiyo.Kwa mujibu wa tafiti hizo Front National kinaweza kujikingia asili mia 30 ya kura na kuwapita wahafidhina wa muungano wa UMP/UDI na chama cha kisoshialisti cha rais Francois Hollande.Pindi chama hicho cha siasa kali za mrengo wa kulia kikishinda,miaka miwili kabla ya uchaguzi wa rais,sura ya kisiasa itabadilika nchini humo.Waziri mkuu Manuel Valls ameonya dhidi ya hatari ya kupata nguvu chama cha Front National.Duru ya pili ya uchaguzi wa mikoa itafanyika Marchi 29 ijayo.