Chama kikuu cha upinzani nchini Sierra Leone kinafikiria kufungua mashtaka dhidi ya Rais Ernest Bai Koroma wa nchi hiyo, na kimesema kitakataa kushirikiana kwa namna yoyote ile na serikali. Hatua hiyo inatokana na jinsi makamu wa rais wa Sierra Leone, Samuel Sam-Sumana alivyofukuzwa kazi. Baada ya mkutano wake wa dharura siku ya Jumamosi, chama hicho kimesema kitaiomba Mahakama Kuu kupitia upya uamuzi wa kufukuzwa kazi Sumana. Wiki iliyopita, Rais Koroma alimfukuza kazi makamu wake, akisema kuwa uamuzi huo ulikuwa muhimu kwa sababu Sumana alifukuzwa kutoka kwenye chama tawala. Makundi kadhaa ya kiraia yamesema hatua hiyo ni kinyume na katiba na Sumana amekata rufaa mahakamani kupinga uamuzi huo. Rais Koroma amemteua Victor Foh, kuwa makamu wake mpya.
23 Machi 2015 - 10:52
Msimbo wa Habari: 678506
Chama kikuu cha upinzani nchini Sierra Leone kinafikiria kufungua mashtaka dhidi ya Rais Ernest Bai Koroma wa nchi hiyo