Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Irna akinukuu kutoka Reuters, Baraka Obama amesema: tufauti zangu na waziri mkuu wa utawala (haramu) wa Israel Benjamin Netanyahu nikuhusu matatizo yaliopo baina ya Israel na Palestina nasi maswala binafsi.
Rais wa Marekani alibainisha kuwa: tofauti zetu zinamsingi wa kisiasa kuhusu suluuu na amani katika mashariki ya kati.
Aidha alisema: taswira yakuwepo mpango wa utatuzi wa taifa la Palestina ili kumaliza tatizo kati ya Israel na Palestina ni suala zito sana, kwani Netanyahu kabla ya uchaguzi uliopita katika zama za utawala wake alipinga kuwepo taifa la Palestina.
Obama aliongeza kusema: mpaka ifikapo mwishoni mwa utawala wangu nitahakikisha kunakuwa na fungamano jema baina ya Israel na Palestina, pia amesema kuhusu muafaka wa mpango wa nyuklia wa Iran kuwa: kufanya muafaka na Iran kuhusu mpango wake nyuklia nisuala zuri kwa amani ya Israel na Marekani.
25 Machi 2015 - 19:25
Msimbo wa Habari: 678971
Baraka Obama Rais wa jamhuri ya Marekani amesema: tofauti zangu na Benjamen Netanyahu sitafauti binafsi bali nitafauti zamsingi